Followers

Total Pageviews

Learn a new language and get a new soul. ~Czech Proverb

Learn a new language and get a new soul. ~Czech Proverb

Sunday, March 6, 2011

BARUA ZA HEWANI ZALETA BLOGU MPYA

Blogu NdimiAfrika tunapiga hodi, Jamaani!

Nilifikiri jina “NdimiAfrika” linafaa kutokana na Kiswahili changu kidogo “ndimi” maana yake ni “TOUNGUES/ LANGUAGES”.

Awali niseme kwamba wazo la blogu hii siyo langu.

Kusema ukweli blogu NdimiAfrika hii itakata roho punde ikiwa wasomaji hawana maoni ya kuchangia wala wanablogu wengine wenye msingi wa lugha ya Kiswahili hawaiungi mkono.(Kwamsemo wa wenzetu itakuwa moja tu ya takwimu za watoto waliyozaliwa tayari kufa (STILLBORN).

Mimi, labda kwa ule utundu wangu, nimethubutu kuanzisha leo kama ishara ya kutoa heshima kwa wale wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili waliyoanzisha wazo ili.


MIMI NA WAO TUNAYO NDOTO KWAMBA KWA KUSHIRIKIANA TUKIWA WAAFRIKA HAPA MTANDAONI TENA CHINI YA NDIMIAFRIKA, TUNAWEZA TUKAMLAZIMISHA KILA MWANDISHI WA KAMUSI YA LUGHA YA KIAFRIKA APITIE BLOGU HII ILA KUKAMILISHA SHUGHULI YAKE YA MAANDISHI YA HIYO KAMUSI IKIWA YA KIZULU, KINDENGELEKO, KIBEMBA, AU LUGHA YOYOTE ILE INAOZUNGUMZWA BARANI KWETU AFRIKA.


Tutakuwa wahariri wengi tu, na kadiri teknolojia inavyoturuhusu, tutaihamisha blogu hii (NdimiAfrika) itoke mikononi mwangu ili iwe yetu sote Wahariri wenzangu; lakini mpaka leo hatujui hao wahariri watakuwa akina nani ki ujumla, lakini tunawakaribisheni wote tu!


Leo nimeona niwapeni mawasiliano yangu na baadhi ya WanaAfrika waliyojishughulisha hadi leo na wazo hili
MANYANYA ANAMWANDIKIA JOHN MWAIPOPO:

John

NITAFANYA RAFIKI YANGU... NA ITAKUWA SHUKRANI KUBWA KWA UPANDE WETU KAMA PROF MATONDO NAYE ATAPATA MUDA KIDOGO KUCHANGIA IKIWEZEKANA.   Yupo tena na ndugu yangu mmoja Baraka Kambi  naye aliyeonyesha moyo baada ya kusoma maandhari yako


Tuliwasiliana na Baraka Kambi kama ifuatavyo:


Manyanya Phiri to Baraka

Kwako Baraka

Lugha gani unaweza kuongea katika kibaraza hicho, Ndugu yangu Baraka?  Mimi binafsi ningeingiza Kizulu labda na Afrikaans ambazo ni lugha mbili kubwa za asili Afrika Kusini.  Ndugu yetu Mwaipopo labda Kinyakyusa.

Tutaanza kwa maneno ya kawaida tu kama KISWAHILI=KIZULU=AFRIKAANS=KINDENGELEKO=?,  "WINGU"="IFU"="VOLK"=""=""
"KIDOLE"="UMNWE"="FENGER"=""="" ,.... na maneno kama hayo.


God bless!
On Sat, Mar 5, 2011 at 3:13 PM,
Baraka Kambi acekque@yahoo.fr
wrote:

Sawa! Kisukuma/kinyamwezi and obviously, kiswahili!

Baraka





KWAKO TENA, JOHN

KINGINE, ITAKUWA TAMU SANA BLOGU YETU TUKIKARIBISHA TENA NA WANAHISTORIA watakaotupatia historia ya watu hao (au makabila) ambao lugha yao tunaijadili, mfano Kizulu.  Na kama hatupati hao wa taalam hata mhariri yoyote wa lugha hiyo katika blogu yetu (NdimiAfrika) anaweza akatupatia kidogo huo ufafanuzi zaidi (HISTORICAL AND ETHNOLOGICAL BACKGROUND) kuhusu jamii hiyo. Kujuwa lugha bila kwelewa historia na utamaduni wa watu hao ni sawa na kuvaa tai huku ukiwa umevaa shati ya mikono mfupi: hujakamilika!


Mimi nimeshaanza kwandika kidogo.  Natumaini kabla ya mwisho wa mwezi huu (MARCH) blogu NdimiAfrika itakuwa mtandaoni, au vipi?


2011/3/6 John mwaipopo <johnmwaipopo@yahoo.com>:


Awali nikuombe radhi kwa kuchelewa kukujibu e-mail yako.
Pili nikupongeze kuwa kuwa msomaji mzuri wa blogu za Watanzania.
Unatutia moyo sana.  Kwa niaba yao nakushukuru.

Kuhusu suala la kuanzisha blogu ya lugha nakubaliana na wewe kuwa wewe na mimi tuanzishe na wengine watafuata na kutukuta huko.

Nadhani pia tumshirikishe Profesa matondo wa blogu ya Matondo.  Yeye ni linguist [MTAALAM WA LUGHA MBALIMBALI&Phiri’s translation] aliyebobea.  Aatatusaidia masuala ya ufundi wa lugha na jinsi ya kufafanua  jambo.

Kwenye ile post yangu ya kuanzisha lugha nimesharekebisha pale kwenye link iliyokuwa haifanyi kazi.


Off [the]point:  Wakati huu nasikiliza wimbo “NGIXOLELE” wa Senzo [Mthethwa na taamka ‘mtetwa’]. Huwa naupenda sana wimbo huu tokea ulipotoka misaka ile ya katikati ya 1990 (nadhani ni 1996-7).  Nakuomba unifafanulie wimbo una ujumbe gani. Ikiwezekana niandikie lyrics nianze kujifunza kizulu kwa kuongea. halafu kuna taarifa zinazochanganya watu kuwa Senzo bado yu hai ama alishakufa.

Jumapili njema

John Mwaipopo

Mbeya Tanzania

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Mwenga! hapa pabwina sana mkitili chabwina sana kuwanzisha blog hiyi ninogela kuyandika gamahele, yatiniyandika ligono lingi.

Goodman Manyanya Phiri said...

Kingoni hicho, siyo, Mkuu? Basi tupe tafadhali tafsiri yake neno kwa neno.

Mimi nitakuwa najua "pabwina sana"= "vizuri sana", lakini maneno mengine giza tu.

Nawe karibu sana kuchangia; tena kwa mawazo yetu ya hapo awali ninaweza kusema tungefurahi kuwa nawe kama moja ya wahariri wetu, NaNgonyani.

Yasinta Ngonyani said...

"Mwenga! hapa pabwina sana mkitili chabwina sana kuwanzisha blog hiyi ninogela kuyandika gamahele, yatiniyandika ligono lingi".MAANA YAKE NI HIVI JAMANI! HAPA PAZURI SANA MMEFANYA VIZURI SANA KUANZISHA BLOG HII NATAMANI KUANDIKA MENGI, NITAANDIKA SIKU NYINGINE.