Followers

Total Pageviews

Learn a new language and get a new soul. ~Czech Proverb

Learn a new language and get a new soul. ~Czech Proverb

Friday, March 11, 2011

UKUBIZWA KOMUNTU KUNGUKUZWIWA NGUMUNTU

"KUTAJWA KWA-MTU NDIYO-KUSIKILIZWA NA-MTU"


Leo tufufunze (kabla hatujaenda mbali) namna ya kutaja watu kwa lugha ya Kizulu
Mimi, Sisi, Wewe, Ninyi, Yeye, Wao

KOTE WAZULU HAPO WANATUMIA   "-na"



MI-na=MI-mi (SWAHILI)
WE-na=WE-we (SWAHILI)
NI-na=NI-nyi (SWAHILI)
YE-na=YE-ye (SWAHILI)

SI UNAONA HAPO JUU TOFAUTI YAKE NA KISWAHILI HAMNA KIMSINGI??
UGUMU UNAKWEPO TU KIDOGO KWA "Wao" na "Sisi"

Bona=WAo (SWAHILI)
Thina=SIsi (SWAHILI)


KWAHERI TENA KWA LEO! JISIKIE HURU KUULIZA MASWALI NA KUTOA MAONI YAKO

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

"KUTAJWA KWA-MTU NDIYO-KUSIKILIZWA NA-MTU" Kingoni kujova kwa munu ndi kupilikiswa na munu.

mimi= Nene
sisi =Tete
Wewe = Veve
Ninye= Nyenye
Yeye = Mwene
Wao = wombi

Swali je nilazima unapotamka upandishe juu? Ahsante kwa somo la leo = Usegwili kwa lisomo la lelu.

Goodman Manyanya Phiri said...

Unapo ongea Kizulu, Mkuu, jaribu kila wakati kucheza na sauti yako kadiri uwezavyo kusudi utofautishe maana ya matumizi ya neno.

Mfano: NGIzoHLALA= "NITAKAA"
Lakini: ngiZOhlala= "NITAKAA HATA USIPONITAKA NIKAE/ NITALAZIMISHA KUKAA"


Asante sana kwa Kingoni. Nami najifunza lugha hiyo kwako "ile mbaya"!

malkiory said...

Somo hili limefanikiwa kwa asilimia 100. Sikujua kama wewe ni mwalimu mzuri hivi, nilijua ni mpiganaji kwenye kudai haki. Niliangalia pia kesi dhidi yako kwenye video. Kwa kweli ulikuwa makini kupambana na jury kwa command kali kabisa ya kimombo. Endelea na moyo huu wa kujitolea kuelimisha jamii.

Goodman Manyanya Phiri said...

@MM, Mkuu!

Inatia moyo kusikia somo linaeleweka. Ni maoni ya kwanza kunitia moyo kiasi hicho. Mimi na ndugu zangu katika wazo hilo (mifano michache akina John Mwaipopo, Yasinta Ngonyani) tutazidi kupata moyo na kutafuta mbinu mpya za kueleweshana uAfrika wetu sote.


Kuhusu mambo ya kortini, hao wananicheleweshea tu lakini hawana haki. Kama sasa hivi, Waziri wangu ameamru juzi ananitaka tena kortini yake ya kijeshi saa mbili za asubuhi Alhamisi 17 March 2011 kujibu mashtaka 10 yale ya zaidi ya miaka 10 sasa (March 9, 2001).

Lakini mashtaka nimekwishajibu katika barua yangu kwa Raisi wa nchi yetu, isipokuwa tu ni kwamba Waziri huyo wetu wa ulinzi hana wakubwa wa kutosha jeshini wa kumshauri hatafanikiwa kwani ziko sheria na korti zingine (mfano LABOUR COURT) vitakaesimamisha tena korti yake ndogo ya kijeshi kwani Afrika Kusini inazo sheria kali sana za kuwalinda wakereketwa (WHISTLEBLOWERS)kazini za serikali wanaopewa mashtaka ya kulipiza kisasi baada ya kutoboa au kufichua ufisadi ndani ya vyombo vya dola kama huyo mpwa (wake Mzee Mkongwe mwenye miaka 27 jela) aliyepata ujemedali kwa kufanya umalaya jeshini mwetu wakati la sivyo angebakia kuwa Meja tu.

Yako mawili au matatu sasa. 1. Wataniwua tu lakini hapo niko tayari kufa kwani ulimwengu utajuwa nimewuliwa na hilo kabila linaojidai limepewa na Mungu kutawala Waafrika wenzao bila elimu bali kiburi tupu.

2. Raisi atamfukuza hivi karibuni Waziri wake huyo wa kike ingawaje walikuwa marafiki tangu zamani enzi za mapigano dhidhi ya Makaburu.

3. Mwaka ujao, chama-tawala kitamwondoa madarakani Mzee huyu Mheshimiwa mwenye wake-sijui-wangapi kama ikiwonekana Waziri wake wa kike anamtawala yeye mwanaume hata pale pasipositahili: penye uvunjaji wa haki za wananchi.

Mimi shwari kabisa rohoni mwangu. NITASHINDA TU! Na Asante sana, Mkuu M.M.!